Wapenzi, tumeanza kula pamoja na watoto wa vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji & yatima. Nina furaha isiyo kifani kuwapikia vyakula vitamuuu vyenye ubora 😋 Ndoto yangu kubwa zaidi ilikua kuweza kugusa maisha ya wengine, namshukuru Mwenyezi Mungu kuweza kufanyika baraka kwa kushare kidogo nilichonacho na watoto yatima. Kama ambavyo watoto wa majumbani hutolewa Out na wazazi/ndugu zao kuonja ladha za vyakula vya nje basi vivo hivyo ni furaha yangu kuupeleka utamu wa vyakula vya nje kwa watoto hawa ambao yawezekana hawapati nafasi hiyo. Kwa uwezo na kibali cha mwenyezi Mungu, nitajitahidi kila itakapowezekana kuwaandalia watoto yatima wa vituo mbalimbali breakfast/lunch au dinner. Kwa wote mnaochangia sehemu ya kipato changu kidogo, wanafunzi wangu wa madarasa pamoja na washirika wangu wote wa kibiashara. Mwenyezi Mungu aendelee kuwabariki, awazidishie maradufu pale mlipotoa mkapate kuongezewa. Tuendelee kugusa maisha ya wengine & kufanyika baraka. Kwa followers wangu, nawashukuru kwa support yenu siku zote. Mwenyezi Mungu awalinde na kuwapatia hitaji za mioyo yenu. NAWAPENDA. #foodloverstz #spreadinglove #sambazaupendo #utamuguaranteed #spreadingsmiles